Wanandoa mwanaume na mwanamke walihamia kwenye nyumba mpya mtaa mwingine.
Asubuhi iliyofuata walipokuwa wakipata staftahi, mwanadada huyo alimwona jirani yake akining’inia kuanika nguo nje.
"Hizo nguo sio safi sana, hazijatakata". Alisema, "hapo kuna mawili, mosi hajui kufua vizuri, pili labda sabuni anayotumia si nzuri".
Mumewe alitazama, akabaki kimya.
Kila wakati jirani yake alipoanika nguo zake, mwanamke huyo mgeni nzengoni alitoa maoni yaleyale.
Wiki moja baadaye, mwanamke huyo alishangaa kuona mabadiliko kwenye nguo anazoanika jirani yake. Akamwambia mumewe, "Angalia, hatimaye amejifunza jinsi ya kufua kwa usahihi. Ninashangaa ni nani aliyemfundisha hili? Au labda kabadilisha sabuni!"
Mume akajibu, "Niliamka asubuhi na mapema na kusafisha madirisha yetu."
Na ndivyo ilivyo kwenye maisha… Tunapotafsiri kile tunachoona tunapotazama wengine kinategemea usafi wa dirisha tunalotazamia.
Ikiwa mtazamo wako wa maisha umetanguliwa na hasira, wivu, chuki, au tamaa zisizotimizwa, hapana shaka utahukumu wengine vibaya. Mambo haya hutia ubongo ukungu.
Kumhukumu mtu hakuelezei yeye ni nani. Inafafanua wewe ni nani.
𝑀𝑤𝑙 𝐿𝑎𝑧𝑎𝑟𝑜 𝐾𝑎𝑣𝑎𝑔𝑒𝑚𝑒.
Social Plugin