1. Jipe uhalisia wa mambo hata kama unauma na hakikisha unauelewa, hapa inahusu kuyajua madhaifu yako na nguvu zako, yakubali madhaifu uliyonayo na amua kuyashughulikia hayo kwanza.
2. Baini ni wapi unataka kuelekea, ni muhimu kuwa na dira ya muelekeo wa maisha yako.
3. Chagua gari litakalokuwesha kwenda uendako kwa haraka pasipo kupoteza umakini, anzia pale ulipo sasa na sio pale ulipotaka kuwapo
4. Tengeneza imani juu ya gari hilo kwamba unaweza kufikia malengo na uiendeleza imani hiyo
5. Kuwa bora kila siku kuliko ulivyokuwa jana.
6. Harakisha mchakato, usikae na kusikiliza maoni ya watu juu ya jambo lako, watakukatisha tama ama watakuchelesha kuanza.
7. Amua kuanza sasa, jambo lililo gumu katika maisha ni kuanza, mara nyingi mwanzo huwa ni mgumu. Ukiona wapo watu walioweza kufanya nawe unaweza kufanya na zaidi ya hapo, suala la muhimu ni kuwa na mtazamo chanya juu ya hicho unachotaka kukifanya. Mawazo yako huzalisha au huua msukumo wako katika kutekeleza jambo fulani. Uamuzi wa maisha tunaoufanya huamua kiasi cha hatua tunazopiga kimaendeleo.
Rafiki yako,
Lazaro.
Social Plugin