Malezi
ya vijana duniani kote yamekuwa na changamoto zake kulingana na wakati
tunaokuwa nao, na athari za madiliko ya kiuchumi na maendelelo makubwa kabisa
ya sayansi na teknolojia ya mawasiliano, vijana kote duniani leo wanao
utamaduni mmoja, namna wanavyovaa, aina ya vyakula wanavyopendelea, aina ya
muziki wanaoupenda, njia za mawasiliano nk. Kwahiyo dunani kote vijana
wanaongea lugha moja na wanaelewana, mitindo ya mavazi, muziki na njia za mawasiliano
vinawaunganisha sana vijana wote wa mijini na wale wa vijijni, wa mataifa ya
dunia ya tatu na yale ya dunia ya kwanza.
Changamoto
kubwa kwa wazazi ni kwamba wao wanataka kuwaamulia vijana wao kila kitu kwasababu
hawawaamini, jambo hili vijana nao hawalikubali, vijana wanataka kuwa huru,
wanataka kuheshimiwa, kuthaminiwa, na kutambuliwa kama watu wazima; lakini pia
vijana hawa wanatawaliwa na hofu wasiyoijua kuhusu kesho yao.
Wazazi
wengi wanasahau kwamba kudai uhuru ni suala la asili la mwanadamu. Ndiyo maana
ni rahisi sana kwa wazazi wengi leo kusikika wakisema “vijana wa siku hizi
hawana adabu”, wanasahau kwamba hata wao walipokuwa vijana wazazi wao walisema
vivyo hivyo juu yao, ni muhimu kutambua kwamba kila kizazi/zama kina watoto,
vijana, na wazee, na majukumu yao pia ni tofauti kwahiyo kila kizazi kiana
vijana wa siku hizi, watoto wa siku hizi, na wazee wa siku hizi.
Majukumu
ya kizazi kimoja kwenda kingine ni lazima yawe tofauti, Rais wa awamu ya pili
ndg A.Mwinyi alipata kusema maneno haya “kila zama na kitabu chake”
Pamoja
na mengi kuhusu changamoto za vijana yaliyoelezwa katika chapisho hili, jambo
kubwa la kuwahimiza na kuwatia nalo moyo vijana ni kuawashirikisha juu ya
mpango mwema wa Mungu kuhusu maisha yao ya sasa na ya baadae. Yeremia 28:11-12.
A. HATUA
ZA UKUAJI WA MTOTO
OEDIPUS NA ELECTROPUS
Tafiti
nyingi duniani kuhusu makuzi ya watoto zinaonesha kuwa watoto wanapofikia umri
wa miaka 3-5 huwa wanaingia kwenye hatua inayoitwa kwa kitaalam PHALLIC STAGE, ambapo
katika hatua hii mtoto wa kiume huwa anamtamani mama-OEDIPUS COMPLEX, na mtoto wa kike anamtamani baba – ELECTRA
COMPLEX.
Hatua
za ukuaji wa mtoto zipo 5, na kila hatua ina kuwa na namna yake ambavyo mtoto
anaifurahia kwenye mwili wake kadri anavyokuwa:-
i.
Oral
stage mwaka 0-1; katika hatua hii furaha ya mtoto inakuwa kwenye midomo yake,
ndiyo maana utakuta kila anachokishika anapeleka mdomoni.
ii.
Anul
stage miaka1-3; katika hatua hii furaha ya mtoto inakuwa kwenye uume/uke, na
kwenye njia ya haja kubwa, hapa mtoto anakuwa anajikojolea mara kwa mara na
kujinyea, na kwa watoto wa kiume huwa wanapenda sana kuchezea uume wao. Ukiona
mtoto anachezea uume wake usimkataze, unapomkataza madhara yake huwa ni kupungukiwa
nguvu za kiume.
iii.
Phallic
stage miaka 3-5; ndiyo hiyo ya watoto kuwatamani wazazi wao kwa tofauti ya
kijinsia
iv.
Latency
stage miaka 5-6; katika hatua hii mtoto anakuwa anapenda sana kufanya kazi za
kiubunifu nyumbani, shuleni, kanisani nk.
v.
Adolescent
stage (first stage) miaka 7-11
Katika
hatua ile ya 3, Phallic stage; Hali ile ya mtoto kumtamani mzazi huweza
kuendelea kwa baadhi ya watu hadi wanapofikia umri wa balehe (puberty) ya mwisho
miaka 12 – 19 kwa wasichana na miaka 14-18 kwa wavulana, na kwa wengine
huendelea hadi wanapokuwa watu wazima kabisa. Hapa utakuta mama anapenda zaidi
watoto wake wa kiume kuliko wakike, na baba anapenda zaidi watoto wake wakike
kuliko wakiume, na huwa hamna sababu inayopimika ya upendeleo huu.
Katika
hali hii kwa baadhi ya wasichana mara nyingi utakuta wanakuwa karibu zaidi na
wavulana/wanaume kuliko wasichana/wanawake wenzao, na baadhi ya wavulana kuwa
karibu zaidi na wasichana/wanawake kuliko wavulana/wanaume wenzao; hii huwa
haijalishi ni eneo gani wapo, wakiwa shuleni, wakiwa kanisani, wanapokuwa
kambi, nk. Siyo kwamba wanakuwa hawana upendo na wenzao wa jinsia sawa na wao,
hapana ni kwavile wanakuwa wanajisikia kuwa huru zaidi wanapokuwa na mtu/watu
wa jinsia tofauti na ya kwake, huwa wanakuwa huru sana kiwango cha kuwaambia na
kuwashirikisha hisia na mambo yao ya ndani sana kuhusu mahusiano yao na wapenzi
wao, mahusiano yao na wazazi/walezi wao, mahusiano yao na waalimu wao,
wachungaji wao, na mahusiano baina yao na ndugu zao nyumbani.
Katika
Biblia upo mfano wa Yakobo, yeye alikuwa anajisikia huru zaidi kwa mama yake
kuliko ilivyokuwa kwa baba yake, Mwanzo
25:28.
Kiujumla
vijana wengi (12-19)wanapokuwa wamefikia umri wa balehe na umri wa kuzidi (19+),
wanakuwa na machaguzi mengi juu ya maisha yao, na hii inatokana na maswali
mengi ya hofu wanayokuwa nayo kuhusu maisha na hali yao ya baadae, na wanapenda
kuwa huru na maisha yao, wanapenda kuona wanathaminiwa na kupendwa. Katika
mazingira haya hujikuta wanakuwa wachaguzi wa watu wa kuzungumza nao ambao huwa
wanahisi kuwa hao ni watu wano waelewa zaidi ya mtu mwingine yeyote hata wazazi
wao, wapo vijana ambao wapo huru na karibu zaidi kwa watu wa nje zaidi ya
walivyo huru kwa wazazi wao na ndugu zao nyumbani. Lakini hii pia inachangiwa
na baadhi ya wazazi ambao huwachukulia watoto wao kwa mazoea.
Wazazi
na waalimu mara nyingi hawapendi kuwapa watoto/vijana uhuru wanaoutaka kwakudhani
kuwa kufanya hivyo ni kuwadekeza na kuwapoteza, kinachotokea vijana
wanaponyimwa uhuru na heshima wanayoitaka ni mgogoro kati ya wazazi na vijana
wao kwa upande mmoja, na waalimu na wanafunzi wao kwa upande mwingine,
kwasababu vijana wataendelea kudai uhuru wao hadi waupate; mfn wa Yesu Lk
2:41-49, na mwanapotevu Lk 15:11ff.
Mara
nyingi vijana wanalaumiwa na wazazi na waalimu wao kuwa wanakiburi, lakini
kumbe wakati mwingine hiyo ndiyo njia yao kujitetea na kudai na uhuru,
tunawaona wana kiburi kwasababu mara zote tunataka wafanye kama tunavyotaka
sisi na kwa njia zetu bila kuwaachia na wao watumie njia wanayoweza kuitumia
kufanikisha jambo lilelile.
Ni muhimu
kuwaelewa, na kuwapa uhuru wao, hii itawasaidia wazazi/walimu kujua uwezo
walionao watoto na wanafunzi wao juu ya masuala fulanifulani ya kimaisha.
Wajibu wetu wazazi na waalimu ni kuwasaidia vijana wakue kufikia kuwa watu
wazima wanaoujua wajibu wao na wanaojitosheleza, wanapofanya jambo wakalikosea
na pengine kuwaumiza wao wenyewe, wakati mwingine watalifanya jambo hilo kwa
umakini zaidi ili kuepusha madhara kwao na kwa wengine, na huo ndiyo
uwajibikaji wenyewe.
Tukitaka
kufaulu katika hili ni muhimu sana kujenga juu ya msingi wa mawazo na maoni
waliyonayo vijana kuliko kuwataka wao wajenge juu ya msingi wa hoja na maagizo
yetu wakati wote. Ukali na vitisho kwa watoto/vijana ni dalili ya kushindwa
malezi.
Mwalimu kuwa zaidi
ya mwalimu; mzazi kuwa zaidi ya mzazi, kuwa menta.
Menta:
Huyu ni
mtu mwenye ujuzi, uelewa mpana na uzoefu katika masuala fulanifulani ya
kimaisha, biashara, kilimo, huduma, na kazi. Wajibu mkubwa wa menta ni
kuwaongoza wengine kufikia matarajio yao. Menta ni mshauri, ni mwezeshaji, ni
kiongozi.
Vijana
ni umri wa kipekee sana, vijana sio watoto na wala si watu wazima, hawapendi
kuwa watoto bali wanatamani kuwa watu wazima, na bahati mbaya sana hawajui
namna gani wafanye ili wawe watu wazima, na watu wawatambue hivyo, hapa ndipo
inabidi mzazi asiwe mzazi tu na mwalimu asiwe mwalimu tu, wawe menta.
Sifa za
menta:
i.
Utayari
wa kuwashirikisha wengine maarifa na ujuzi alionao pasipo kuwabagua jinsia,
kabila nk.
ii.
Rafiki
iii.
Mwenye
kusikiliza zaidi ya anavyoongea
iv.
Mwenye
mtazamo chanya kimaisha kwake mwenyewe na kwa anaowaongoza
v.
Kujidhabihu
kwaajili ya wengine
vi.
Mwenye
uwezo mkubwa katika kujieleza na mawasiliano
vii.
Mwenye
kufurahia kufanya anachokifanya
viii.
Mwenye
kujiendeleza kupata maarifa mapya
ix.
Mwenye
uwezo wa kutatua migogoro
x.
Anayejiamini
xi.
Mwenye
kuheshimu mawazo na mitazamo ya wengine na kukubali jitihada zinazofanywa na
wengine
xii.
Mkweli
na mwenye kutimiza ahadi
xiii.
Anayeza
kujifunza kutoka kwa wengine (si mjuaji wa kila kitu)
Hizi
sifa zote, wazazi na waalimu wote wa vijana wanapaswa kuwa nazo, tukiwa nazo
watoto/vijana, na hata watu wazima watatufuata wao wenyewe pasipo kulazimishwa
na mtu. Unafuatwa na mtu kuombwa ushauri ama muongozo, tumia nafasi hiyo
kikamilifu kumfanya huyo kuwa mwanafunzi wa Yesu.
KUFANYA NA VIJANA
|
Anza na yale yenye kuleta
matokeo hasi
|
Michezo kwenye mazingira
rafiki
|
|
Tumia nguvu ya ubunifu
|
|
Washughulishe kwenye mambo
makubwa ya kuleta heshima
|
|
Uwe mkweli, ndiyo yako iwe
ndiyo na hapana yako iwe hapana; kataa ama kubali ukionesha heshima
|
|
Kusikiliza ni kipaumbele
|
|
Wekeza katika nguvu za vijana
|
|
Usiwafanyie, fanya pamoja nao
|
|
B. KUWAJENGEA
VIJANA UWEZO
Tunahitajika
kuwajengea vijana uwezo kwa kuanza na vitu, mtazamo, karama, ujuzi, na hatua
waliyonayo kwa kwakati huo. Kuwajengea uwezo ni suala la muhimu sana kwakuwa
itawasaidia kujiamini , kujiheshimu na kuondoa ile hofu wanayokuwa nayo juu ya
wakati ujao, kuhusu ajira, mahusiano, hali yao ya kiroho, uchumi nk.
Tunapowajengea
uwezo vijana, kwenye suala la ajira, ni muhimu sana kuwapanua mawazo ili kwamba
wanapotazama soko la ajira waone kuwa ni kitu wanachoweza kuanzisha wenyewe
mmoja mmoja ama kwa kujiunga kwenye vikundi kwamaana ya kujiajiri wenyewe na
kuajiri wengine. Tangu zamani za ukoloni vijana wengi waliopelekwa shuleni
walikuwa wanasisitizwa na wazazi na waalimu juu ya kusoma kwa bidii wapate
alama nzuri ili wapate ajira nzuri serikalini na kwenye makampuni, mtazamo huu
umeendelea kuwepo hadi sasa kwenye jamii nyingi nchini mwetu, na Afrika. Wapo wazazi wanaowahiza vijana wao wasome kwa
bidii wapate alama nzuri ili waajiriwe, kwa hiyo vijana walio wengi sana
wanawaza kuajiriwa tu.
Asilimia
70 ya vijana wenye miaka kati ya 13 na 34 ambao ndiyo wengi zaidi kati ya idadi
ya watu milioni 45 waliopo Tanzani ni kundi kubwa ambalo ni tegemezi na hawana
ajira. Hii ni kati ya nguvu kazi ya vijana milioni mbili na nusu amabo wako
mijini na hawana kazi.
Hivi
sasa vijana zaidi ya 30,000 wanahitimu katika vyuo mbalimbali na wengi
wakiishia mitaani kwa kukosa ajira. Sasa hawa ni wa vyuo, wapo wengine
walioshia darasa la saba, wapo walioishia kidato cha nne na sita, na kuishia
huko huko mitaani huku wakiwa hawana ujuzi wowote.
Kutegemea
kuajiriwa kwa sababu zozote zile sio kitu kibaya, lakini pia kutegemea
kuajiriwa kwasababu yeyote ile ni kubaya. Mawazo ya kutegemea kuajiriwa siyo
mawazo yenye afya sana na inafaa yafutwe kwa vijana na miongoni mwa wanajamii
tulionao, wapo vijana wengi mtaani ambao wamechanganyikiwa na hawajui la
kufanya kwakuwa soko la ajira ni gumu sana, hivyo wengi wamejiingiza kwenye
vitendo hatarishi, kama ukahaba, matumizi ya madawa ya kulevya, uhalifu, nk.
Nukuu:
Kama yai livunjika kutokana na
nguvu za nje huharibika, kama yai livunjika kutokana na nguvu zitokazo ndani
maisha huendelea; mambo makubwa hutokea kuanzia ndani ya mtu na siyo nje.
C. MUDA/WAKATI
(time management)
Ni
muhimu sana watoto na vijana wakawa na uelewa mkubwa kuhusu namna ya kutumia muda vizuri (kuukomboa wakati)katika kufanikisha malengo
ya maisha ya kila siku pamoja na kuziishi
ndoto za maisha yao. Ni lazima wafunzwe kanuni/mbinu za kuukomboa
wakati.
Kila
mtu anaishi ndani ya masaa 24, hakuna mtu mkwenye muda wake zaidi ya huo, sote
tuna masaa sawa ya mchana, na masaa sawa ya usiku. Kutumia muda vizuri
inamaanisha kuamua ni namna gani uantumia muda ulionao kupata unachokitataka,
kutumia muda vizuri haimaanishi kuwa bize wakati wote. “Muda ni zawadi kutoka
kwa Mungu na katu haiwezekani kuurudisha nyuma ukipita” – David and Janet Cunningham
Lengo
kubwa la kujifunza namna ya kutumia muda vizuri ni ili kuongeza ufanisi na
uzalishaji.
Matumizi
sahihi/mazuri ya muda husaidia:-
i.
Kuongeza
utulivu
ii.
Kupunguza
msongo wa mawazo
iii.
Kuridhika/kujiridhisha
iv.
kupumzika
kanuni
za kutumia muda vizuri:
i.
Mpango
kazi: “kupanga ni kuchagua”, “kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa”; unaweza
kutumia muda mwingi kuweka mpango kazi wa siku, mwezi, kota, mwaka, nk. Lakini
hiyo itakusaidia kukamilisha majukumu yako kwa ufanisi. Mpango kazi ni muhimu
ukawa na muda/saa, shughuli, ikibidi na muhusika, mfano
9:00asubuhi
– 11:00asubuhi chai
11:00asubuhi
– 12:00mchana kujisomea kitabu
ii.
Nidhamu
ya muda: panga mpango kazi na kasha ufanyie kazi mpango huo, usipoutekeleza
mpango wako ni bure.
iii.
Kuweka
vipaumbele:- Unapokuwa na mambo mengi ya kufanya na unataka kuyafanya yote kwa
pamoja, hautaweza hadi utakapoyagawa mambo yako katika vipande vidogo vidogo
kutoka na umuhimu wake (importance) na uharaka wake(urgency). Unapoweka
vipaumbele inajkusaidia kuanza na mambo yenye kuhitaji uharaka na yale ya
muhimu.
Mtalaam
wa masuala ya uchumi na soshologia Vifredo Pareto kwenye kanuni yake ya 80/20
anasema kuwa 80% ya matokeo yanayopatikana inatokana na 20% ya kazi
iliyofanyika. Hii inamaanisha kwamba mtu anapokuwa na mambo kumi(10) ya
kufanya, atarajie mafanikio kwa 80% kwa kutekeleza mambo mawili(2) tu ya muhimu
kati ya hayo kumi.
iv.
Sema
hapana: Haiwezekani ukafanya kila kazi, unapokuwa umepanga mambo yako kuyafanya
akatokea mtu mwingine na kukuingizia ratiba/jambo lake sema hapana.
v.
Jitenge
na vipoteza muda: vitu hivi ni vitu
muhimu kwenye maisha yetu lakini kwakweli hutupotezea sana muda, mfn utazamaji
wa TV usio na mpango/uliopitiliza, maongezi yasiyo na faida, vikao visivyo vya
muhimu, wageni wasio na mpangilio, simu na meseji, kuahirisha ahirisha mambo,
kuendekeza usingizi, kutafuta vitu usivyokuwa na uhakika wapi vipo, kusubiria
huduma unayoweza kuipata mahali pengine. Hapa unaweza kuwaachi vijana nao
waeleze ni mambo gani yanayowapotezea muda.
vi.
Kasimisha(delegating):
Unapompa mtu mwingine wajibu wa kufanya majukumu yako huku ndiyo kukasimisha.
Unapokasimisha madaraka ni muhimu kuchagua mtu mwenye uwezo kufanya ambavyo
ungefanya wewe.
vii.
Malengo:
Ni lazima kujiwekea malengo ya namna utakavyo ikamilisha kazi yako, na kichwani
uwe na picha kamili (picturise)ya namna kazi itakavyokuwa. Unaweza kupanga
malengo ya muda mfupi nay a muda mrefu.
BI. MGAWANYO WA
SHUGHULI KULINGANA NA UMRI NA MUDA TULIONAO
ZABURI 90:10
Siku za miaka yetu ni miaka 70,
Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, maana
chapita upesi.
i.
Umri
wa kukua 0-25
ii.
Umri
wa mazalisho 25-60
iii.
Umri
wa kupumzika na kula matunda ya kazi yako duniani 60-70
iv.
Kuishi
paradiso kuanzia miaka 70
B2. MAISHA YETU
KAMA SAA
§
Miaka
70 ndani ya masaa 24
§
Miaka
20=11asubuhi;
§
Miaka
25 = 12 mchana
§
Miaka
30 = 1 mchana
§
Miaka
35 = 2 mchana
§
Miaka
40 = 4 jioni
§
Miaka
45 = 5 jioni
§
Miaka
50 = 6 jioni
§
Miaka
55 = 8 usiku
§
Miaka
60 = 10 usiku
§
Miaka
70 = 12 usiku
Pamoja na kwamba tunao muda
sawa, bado watu husema na kulalamika kuwa “muda hautoshi”
Basi utujulishe
kuzihesabu siku zetu, tujipatie moyo wa hekima. Zaburi 90:12
Lazaro JP Kavageme,
Founder, Inuka Tuondoke Ministries
Founder, Inuka Tuondoke Ministries
Project Director at Child
Development Center TZ 555
Mob:0787-654724/0769-085178
Inukatuondoke.blogspot.com
Jan 2017
Social Plugin