Usiache kuomba, usikate tamaa!

Kupitia shinikizo la hewa (pressure) na muda (time), mchanga hugeuka kuwa Lulu na makaa kuwa Almasi.
Ni sawa na vile maji ya moto hulainisha kiazi lakini maji hayohayo ya moto hulifanya yai kua gumu.
Jambo la muhimu sio kile tunachopitia bali ni vile tumegeuka na kua baada ya kupitia kile tulichopitia.

Luka 18:1 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.

Usiache kuomba, usikate tamaa. Hauwezi kujua umebakiza hatua ngapi kufikia hatima ya kile ulichokipambania kwa muda mrefu. Yesu alisema; Lakini fahamuni neno hili, Kwamba mwenye nyumba angalijua saa atakayokuja mwivi, angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa. Luka 12:39

Kuna hatua hauwezi kuistahimili na utapwaya ukiwa Mchanga ni hadi uwe Lulu, kuna hatua hauwezi kuistahimili na utapwaya ukiwa Makaa ni hadi uwe Almasi; kuna mahali hauhitajiki na utapwaya ukiwa kiazi kibichi ni hadi uwe kiazi kilichoiva, kuna mahali hauhitajiki na utapwaya ukiwa yai bichi ni hadi uwe yai lililochemshwa; nyakati ngumu unazopitia ni mchakato kukusogeza kwenye hali ile utakayokubalika mahali Mungu anapotaka uwepo, yeye hawezi kukuweka mahali ambapo utapwaya.

Usiache kuomba, usiache kupiga hatua kwenda mbele, wala usikate tamaa!