Moyo

Moyo wako haukatai chakula tu;  pia unakataa nishati hasi (negative energy).  Ikiwa moyo wako utaanza kukataa sehemu fulani, watu fulani, au vitu fulani; usikilize na uuamini.

Uwanja wa sumaku wa moyo (the heart"s magnetic field) una nguvu mara 5000 zaidi kuliko uwanja wa sumaku wa ubongo. Unavuta watu, uzoefu, mahali, na nishati inayolingana na mtetemo/muelekeo wa mawazo, maneno na hisia zako.

Kila kitu unachosema, kila wazo chanya unalofikiria, linaimarisha uwanja wa sumaku wa moyo. Unapozungumza maneno ya shukrani, upendo, na utoshelevu, unachaji nguvu hiyo ya sumaku kwa nishati chanya, kadri nguvu ya usumaku ya moyo inavyokuwa imara ndivyo unavyoweza kuvuta vitu vizuri kukujia. Moyo wako hausukumi damu tu, unakataa vitu, na unavuta; ni sumaku.

Sayansi inaonesha pia kwamba moyo una neuriti 40, hizi ni nyuzi maalum za neva ambazo huunda sehemu ya mfumo wa neva wa ndani wa moyo, unaojulikana pia kama "ubongo mdogo." Hii inamaanisha kwamba ndani ya moyo kuna ubongo.

Mithali 4:23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Kwenye Wafilipi 4:8, Paulo mtume anashauri watu wafikirie na kujiwazia mambo mazuri mazuri maana hayo huimarisha uwanja wa sumaku wa moyo na hivyo huvuta mambo mazuri kumdhihirikia mtu.

Yesu anasema...
Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake. Luka 6:45

Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Warumi 10:10

Tenzi namba 55 "Nipe Moyo wenye Sifa, siyo wa utumwa"