Barazani kwa mfalme Sulemani kuna wanawake wawili ambao wameleta kesi ya kifo cha mtoto mmoja kati ya wawili waliozaliwa na wanawake hao. Mfalme anaelezwa kwamba usiku uliopita wakiwa wamelala mmoja wao alimlalia mtoto wake kwa bahati mbaya na akafa, aliyeua mtoto wake akambadilisha mtoto wake kwa kumuweka upande alipolala mtoto mzima wa mwenzake. Wanapoamka asubuhi mwanamke aliyebadilishiwa mtoto anagundua kwamba mtoto aliyelala ubavuni pake amekufa, anapomchunguza kwa kumlinganisha na yule aliyelala ubavuni pa mwenzake anagundua kwamba mtoto aliyekufa si wa kwake bali ni yule aliye hai. Kesi ikawa ngumu mwisho wanafikishana barazani kwa mfalme.
Katika kutafuta suluhu, mfalme anaamua atamkata katikati mtoto aliye hai kisha awagawie wanawake wale kila mmoja kipande kimoja, mwanamke mmoja anakubaliana na uamuzi huu lakini mwingine anakataa na kushauri kuwa kuliko mtoto kuuawa ni akheri apewe mwenzake mtoto huyo, mwanamke aliyefiwa mtoto anasisitiza mtoto akatwe vipande viwili vigawanywe baina yao wawili. Katika mazingira haya mfalme anabaini ukweli kwamba mwanamke asiyetaka mtoto akatwe vipande viwili ndiye mama yake na yule mwingine siye. Hivyo mtoto aliye hai anakabidhiwa kwa mama yake. 1 Wafalme 3:16-28.
Huu ndio msingi wa kitu kinaitwa Nadharia Mchezo (Game Theory)
Nadharia hii ni tawi la mahesabu linalofunza mbinu ya kufanya maamuzi katika mazingira ambayo yanategemea matendo ya watu wengine.
Katika huduma, ujasiliamali, soko la ushindani, na maisha kwa ujumla, kufanya maamuzi sahihi lazıma uzingatie matendo ya wengi na kuweka mpango unaokuhakikishia wewe kupata matokeo mazuri bila kuathiriwa na matendo ya watu wengine. Ukishaelewa mbinu hii, inakusaidia hata kutabiri tabia za watu wengine.
Lazaro Kavageme
Inuka Tuondoke Ministries
Mwanza - TZ
Social Plugin