Ayubu aliamka asubuhi na mapema akaomba kwaajili ya watoto wake, alijenga madhabahu kwa ajili ya kila mmoja wa watoto wake, akatoa sadaka kwa niaba yao.
Ayubu alimwomba Mungu awaangalie wanawe na binti zake, awatakase, na kuwaweka sawa mbele ya kiti chake cha enzi.
Ni ibada ya utulivu iliyoje. Ni heshima iliyoje. Ni Uaminifu ulioje. Aliyafanya yote haya kabla ya dhiki kuu ya maisha yake.
Na siku za karamu zilipotimia, Ayubu alikuwa akituma watu na kuwaweka wakfu, naye alikuwa akiamka asubuhi na mapema na kutoa sadaka za kuteketezwa kulingana na hesabu yao wote. Kwa maana Ayubu alisema, Labda watoto wangu wamefanya dhambi, na kumlaani Mungu mioyoni mwao. Ndivyo Ayubu alivyofanya siku zote. Ayubu 1:5
Ayubu alijua kwamba juhudi zake za malezi zilikuwa na matokeo sawa na huruma ya Mungu…na bado ukweli huo wa ajabu ulimchochea kutumia imani yake zaidi. Alibaki kuwa uwepo wa kudumu katika safari ya imani ya watoto wake, akiilinda mioyo yao si kwa mafundisho yake tu bali kwa maombi.
Ungana nami..
Tuombe kwa imani ya Ayubu, tukijitayarisha kwa lolote linalokuja kinyume na watoto wetu, licha ya malezi bora na mafundisho tunayowapatia kila siku.
Sala Kwaajili Ya Watoto Wetu
Baba wa Mbinguni, mfalme wa Utukufu,
Wewe uliye hodari kuliko tunavyoweza kueleza. Jinsi Wewe ulivyo mkuu! Wewe peke yako ndiwe mtakatifu. Wewe peke yako unatufanya wapya na kutufanya Wako.
Ninamwinua mtoto wangu kwako ee Bwana, na kuutoa moyo wangu kwako. Damu ya Kristo imtakase, dhambi zake zitupwe katika vilindi vya bahari (Mika 7:19). Na amkaribishe Mwokozi wake rohoni mwake. Na aone huruma Yake, neema yake na ukweli, na kuvithamini hivyo zaidi kuliko kitu kingine chochote! (Mathayo 6:21)
Na amfurahie Muumba na Mfalme Wake, na kutamani kukutumikia Wewe siku zote za maisha yake. Wimbo Wako na ukae juu ya roho yake (Zaburi 118:14), Neno Lako na liwe nanga akilini mwake. Amani yake na itokane na wokovu Wako, furaha yake na itokane na sifa Zako.
Uulinde utu wake, na ulinde moyo wake na majaribu. Afanye kazi kwa unyenyekevu na atembee kwa ujasiri katika imani!
Ushindi unapokuja akuabudu, inapokuja shida na aendelee kukuabudu. Anapokosa maarifa, anapokosa hekima, ongeza hofu yake kwako na umsogeze Kwako kwa imani kamili (Yakobo 1:5). Anapokandamizwa, mkaribie kwa faraja. Anapotanga-tanga, na umreheshe (Luka 15).
Bwana, nipe uwezo wa kumtunza na kumpenda kama Wewe, nimuelekeze Kwako kila hatua ya njia. Bwana, nikumbushe daima kwamba yeye ni wako. Wako wa kufinyanga, umtumie kwa utukufu wako.
Naomba nimkabidhi Kwako, kila siku. Nisamehe wakati moyo wangu unapowaza njia zake, badala ya kusikiliza mpango Wako kamili. Uhai wake uko mikononi Mwako, naomba na kuamini.
Amen.
Social Plugin