Jenga jina, heshima, na ufalme wako juu ya msingi wa upendo kwa watu wengine.

Napoleon Bonaparte anaandika

"Alexander, Kaisari, Charlemagne na mimi mwenyewe tulianzisha milki kuu; lakini mafanikio ya fikra zetu ulitegemea matumizi ya nguvu ya majeshi. Yesu peke yake ndiye alianzisha na kuujenga ufalme wake pasipo kutumia nguvu za majeshi bali upendo, na hadi leo hii mamilioni watakufa kwa ajili yake, nadhani ninaelewa kitu cha asili ya mwanadamu; nami nawaambia, hawa wote walikuwa wanadamu, nami ni mwanadamu; hakuna mwingine aliye kama yeye; Yesu Kristo alikuwa zaidi ya mwanadamu. Nimewatia moyo watu wengi kwa ibada yenye shauku kiasi kwamba wangekufa kwa ajili yangu lakini kufanya hivi ilikuwa ni lazima niwepo kwa uwazi na ushawishi wa umeme wa sura yangu, maneno yangu, na sauti yangu. Nilipowaona wanaume na kuongea nao, niliwasha moto wa kujitolea mioyoni mwao. Kristo peke yake ndiye aliyefaulu kuinua akili ya mwanadamu kuelekea yasiyoonekana. Yesu Kristo alihitaji kitu ambacho ni vigumu sana kukidhi kwa akili ya kawaida; Anahitaji kile ambacho mwanafalsafa hawezi kukipata hata kwa msaada wa marafiki zake, wala baba kwa watoto wake, au mke kwa mume wake, au dada kwa kaka yake. Anahitaji moyo wa mwanadamu. Anaudai bila masharti; na mara moja matakwa yake yanatimizwa. Ajabu! Kwa kuupuzia wakati na kujikana, roho ya mwanadamu, pamoja na nguvu zake zote na uwezo wake wote, inakuwa kiungo cha ufalme wa Kristo. Wote wanaomwamini Yeye kwa dhati, huona upendo huo wa ajabu, usio wa kawaida kuyoka kwake. Jambo hili ni zaidi ya upeo wa uwezo wa ubunifu wa mwanadamu. Mabadiliko ya nyakati hayana uwezo wa kuzima moto huu mtakatifu; wakati hauwezi kumaliza nguvu zake wala kuweka kikomo kwa upeo wake. Hiki ndicho kinachonigusa zaidi; Mara nyingi nimeifikiria. Hili ndilo linalonithibitishia kwa hakika kabisa Uungu wa Yesu Kristo.”

Napoleon aliandika nukuu hii kuelekea mwisho wa maisha yake alipokuwa katika hali ya kutafakari akiwa kifungoni katika kisiwa cha St. Helena.

Nukuu hii kutoka kwa Napoleon Bonaparte inaonyesha utambuzi wa kina wa nguvu ya kipekee na ya kudumu ya upendo. Wakati Napoleon, pamoja na Alexander, Caesar, na Charlemagne, Farao, walianzisha milki kubwa kwa kutumia nguvu, tawala zao zilikuwa za muda na mara nyingi zilipingwa, kinyume chake, Yesu Kristo, kulingana na Napoleon, alijenga "ufalme" usiotegemea nguvu za kimwili au hofu kwa watu, bali juu ya upendo, mafundisho ya wema, msamaha, na unyenyekevu. "dola" hii ya kiroho imeendelea kwa zaidi ya miaka elfu mbili na inaendelea kuhamasisha na kugeuza maisha ya mamilioni ya watu duniani kote, kuonyesha ushawishi mkubwa, wa kudumu wa upendo na maadili ya kiroho. Nukuu hii inasisitiza wazo kwamba nguvu na ushawishi wa kweli huja kwa upendo na ufahamu, sio mabavu au sheria.

Jenga jina, heshima, na ufalme wako juu ya msingi wa upendo kwa watu wengine. 

Matendo 5:27-41
Mathayo 5:16, Warumi 12:10