Usiruhusu maneno ya adui yakuvuruge.

Historia inamtaja Neil Alden Armstrong kuwa ndiye mtu wa kwanza kutua mwezini mwaka 1969.

Neil anasimulia kisa hiki; 
Wakati akiwa kijana mdogo kwenye mtaa aliokua akiishi na familia yake, palikuwa na jirani zao mume na mke ambao mara nyingi walikua wakigombana, na anasema mke wa huyo jirani yao ndiye aliyekua kisirani sana na aliichukia sana familia ya Armstrong. Anasema siku moja akiwa anacheza nje ya nyumba yao, kwa nasibu mpira wake ulikwenda hadi kwa hao jirani zao watata, alipoufuata akasikia kuna mzozo mkubwa unaendelea ndani kati ya mume na mke, anasema alimsikia mume akimsihi mke wake amheshimu na ampende lakini mke alisikika akiongea kwa jazba na kuapiza kwamba atampenda na kumuheshimu mumewe siku ambayo kijana wa Armstrong (Neil) atakapokanyaga mwezini.. 

Neil anasema, maneno yale yalimtoka yule mama kwasababu ya chuki aliyokuanayo dhidi ya familia ya Armstrong na si kwamba alikua akimtakia mema Neil. Miaka mingi baadae kweli Neil akatua mwezini. 

Kuna muda adui yako anakunenea baraka tena kwa gharama zake mwenyewe huku akidhani anakulaani. Chukua maneno hayo katika uchanya, usiruhusu yakuvuruge. 

Neil Alden Armstrong alikuwa mwanaanga na mhandisi wa anga wa Marekani, na mtu wa kwanza kutembea juu ya Mwezi. (Kuzaliwa Agosti 5, 1930, kufariki Agosti 25, 2012) 

Zaburi 42:5 Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.