Kuna kitu fulani unafanya, kuna maombi fulani unayaomba na
unatamani kuona matokeo yake sasa na hayaonekani; usiche, endelea, na endelea
kukiri uwepo wa matokeo japo hayaonekani; kuna mchakato unaendelea usiouona
utakaoleta majibu ya maombi yako, utakaoleta heshima unayoistahili.
Tunajifunza
kwa Yoshua kwa habari ya kukiri uwepo wa matokeo hata kama hayaonekani sasa,
Yoshua alinena maneno ambayo yalikuja kitimia baada ya miaka takribani 600
baadae; Yoshua 6:26 maneno haya ni ya Yoshua wakati Israel wanaingia Kanaan,
yakaja kutimia wakati wa Wafalme wa Israel, Wafalme wa kwanza 16:34
Tunajifunza
kutoka kwa Daniel aliyeomba kwa muda wa siku 21 ndipo akapokea majibu yake,
wakati anaomba kuna mchakato ulikua unaendelea, majibu ya maombi ya Daniel
yalikuwepo tangu siku ya kwanza ya maombi; Malaika mwenye majibu ya maombi ya
Daniel alikuwa anapambana na mkuu wa anga la Uajemi ili amfikiahie Daniel
majibu yake, laiti kama Daniel angelikata tamaa asingelipokea majibu ya maombi
yake na kumbe mchakato ulikuwa unaendelea. Daniel 10:12
Tunajifunza
kwa mti wa Moso(bamboo) hurefuka hadi kufikia mita 27 ndani ya wiki sita tu na
hapo ndipo huwa umekomaa tayari kwa kuvunwa, mmea wake baada ya kuchipuka huwa
unakua kwa futi moja na nusu hadi mbili kwa siku, lakini kabla ya kuchipuka
mbegu ya Moso hukaa ardhini kwa miaka mitano, ndiyo, miaka mitano. Kuchipuka na
kukua kwa haraka kwa mti huu ni kwasababu ya kujiimarisha ardhini kwa muda wa
miaka mitano, (mchakato).
Kuna
mchakato usiouona unaendelea, jiamini katika hicho unachokifanya, muamini na
umtumaini Mungu, kisha kiri kana kwamba imekwishakufanyika. Usikiri unachokiona
sasa bali kiri kile usichokiona kana kwamba unakiona sasa, Warumi 4:17.
Social Plugin