OMBA NA PIGA HATUA


Luka 11:9 Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.

Luke 11:9 So I say to you, Ask and keep on asking and it shall be given you; seek and keep on seeking and you shall find; knock and keep on knocking and the door shall be opened to you.

Tazama pia..
Luka 18:2-4. Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu. Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu. Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,

Watu wengi hudhani kwamba kumuomba Mungu afanye jambo fulani kwenye maisha yao inatosha; haitoshi hiyo kuna namna inabidi mtu achukue hatua kufanya kitu baada ya hatua ya kwanza ambayo ni maombi. Kwenye injili ya Luka 11:9 anasema kuna kuomba, kuna kutafuta, na kuna kubisha mlango; hizi ni hatua kuelekea kupata kile akitakatakacho mtu.

Kwenye Luka hiyo hiyo sura ya 18:2-4, kuhusu mjane na kadhi, kwamba mjane yule hakuishia kufanya maombi na kukaa nyumbani akisubiri Bwana atende, la, alikua akienda kwa kadhi mara kwa mara kudai haki yake. Fikiri nini kingetokea kama angalikaa tu nyumbani kwake pasipo kuchukua hatua kuenda kwa kadhi? Ni wazi asingelipata hitaji lake.

Tuache uvivu na uoga wa kutotekeleza wajibu wetu kwa kujificha nyuma ya maombi, na kusema tunamuachia Mungu; kuna sehemu ya Mungu kutenda na kuna sehemu ya mwanadamu kutenda ili matokeo yatokee, tuombe na tuchukue hatua kufuatia haki yetu.