HALI YA MOYO BAADA YA TUSI, KRISTO FUNZO LETU


HALI YA MOYO BAADA YA TUSI, KRISTO FUNZO LETU.
.
Kutukanwa ni jambo moja, kutukanika ni jambo lingine. Kazi ya tusi lolote duniani ni kuiharibu hali ya moyo wa mtu na kuitawala, tusi huwa halina uhusiano na mtukanaji bali tusi huwa na uhusiano na mtukanwaji. Unapotendewa jambo baya na mtu uliye na mahusiano naye jambo hilo huuma sana kuliko jambo hilo hilo ukitendewa na mtu usiye na mahusiano naye. .
Tusi linalouma sana ni lile lenye uhusiano na mtukanwaji, tusi lisipohusiana na mtukanwaji halina nguvu juu ya hali ya moyo wa mtukanwaji, ndiyo maana atukanaye huumia sana akiona mtukanwaji hajatukanika, yaani hali ya moyo wa mtukanwaji haijapo haribika, ya mtukanaji ndiyo uharibika. Ukitukanwa na usitukanike maana yake ni kwamba tusi lile halina uhusiano na wewe bali lina uhusiano na mtukanaji. .
.
Tusi linapoiharibu hali ya moyo wa mtukanwaji na akachukua hatua maana yake ni kweli mtukanwaji ana uhusiano na lile tusi na hivyo kule kuchukua kwake hatua ni kutaka kuonesha namna anavyohusiana na lile tusi. Kila kuhusiana huoneshwa hadharani, kuhusiana kusikooneshwa hadharani hakuna nguvu.
.
Ukitukanwa usitukanike, dhamira ya mtukanaji haina nguvu kulifikisha tusi kule linakokusudiwa lifike; mwenye nguvu ya kulifikisha tusi linakokusudiwa lifike ni mtukanwaji. Mtukanwaji anapotukanika anampa mtukanaji uhalali wa kumtawala, na mtawaliwa daima hufanya lile alitakalo mtawala.
.
Katika mazingira yeyote yale, daima mtukanaji ndiyo huwa mwenye inda wala si mtukanwaji.
.
Mtukanwaji asipotukanika, tusi humrudia mtukanaji.
.
1 Petro 2:23 Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
#Jimbi tawikia jimbi, awikapo tawikia#