KILA KITU NI KUTOKA NDANI KUJA NJE.

Kila jambo alitendalo mtu lina mzizi wake moyoni, na hali ya moyo wa mtu ndiyo huamua mwisho wake.

Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.

Mathayo 5:8

Kwa maana alisema moyoni, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona.

Mathayo 9:21

Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano; Mathayo 15:19
Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. Mithali 4:23
Ee Mungu, uniumbie moyo safi,Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu.

Zaburi 51:10
Soma kisa hiki....
Lugano alikuwa anaosha gari yake, jirani yake Steven akamuuliza
Steven: "Jirani, umenunua lini gari yenye thamani kubwa hivi?"
Lugano: "Nimepewa na kaka yangu"
Steven: "Ninatamani ningekuwa na gari kama hii".
Lugano: "Usitamani kuwa na gari kama hii, tamani kuwa na kaka kama kaka yangu".

Mke wa steven ambaye alikuwa anasikiliza maongezi yale pasipo wao kujua akasema "ninatamani ningekuwa huyo kaka
Usitamani vitu ama watu, tamani moyo wa mtu anayefanya mambo yanayokuvutia, hauwezi kuwa kama mtu fulani kama hauna moyo kama wa kwake, kila kitu wakifanyacho watu na vile walivyo mzizi wake upo moyoni, japo kuna gharama kubwa kuwa na moyo kama wa mtu mwingine ila kutamani ni hatua moja kuelekea kuwa nao. Mshirikishe Mungu analo jawabu.

Barikiwa