Kwenye mpira wa miguu kuna kanuni moja inasema "the best way to deffend is to attack" kwa tafsiri ya kiswahili isiyo rasmi ni kwamba "njia bora ya kuzuia mashambulizi ni kushambulia", ukitaka usishambuliwe basi wewe shambulia. Kushambulia ni kuzuia.
Kuna uwezekano waliotunga kanuni hii walisoma maandiko matakatifu (Biblia), wakatumia mawazo na mafundisho ya Kristo Yesu kwa wanafunzi wake;
Siku ile usiku kule bustanini Getisemane, Yesu aliwaambia wanafunzi wake wakeshe wakiomba wasije wakaingia majaribuni, *Mathayo 26:41* hakuwaambia waombe kwasababu wapo majaribuni au waombe watakapojaribiwa; alisema ombeni msije.....
Zuia mashambulizi kwa kushambulia. Usiposhambulia utashambuliwa, unavyozidi kushambuliwa ndivyo unavyozidi kuchoka, na kadri unavyoendelea kuchoka ndivyo unavyoendelea kupoteza umakini na uwezo wa kumzuia adui, na mwishowe utafungwa;
Sasa Kufungwa sio kitu kizuri, hakuna timu inayoshangilia baada ya kufungwa, ukifungwa unadharaulika, unabezwa, unazomewa, na unadhihakiwa; kwakweli kufungwa ni karaha sana, ndiyo maana huwa kuna kamati ya ushindi ama bechi la ufundi. Pamoja na kwamba kwenye mchezo wa mpira kuna matokeo aina tatu, kwamba 1. kushinda, 2. kushindwa, na 3. suluhu; huwa hamna timu inayojiandaa kushindwa ama kutoka suluhu, kila timu hujiandaa ili kuishinda timu pinzani na.
Kadri timu inavyoshambulia ndivyo inavyozidi kugundua adui yake ni dhaifu eneo gani, beki gani anavuja, na eneo gani ni imara, hii huipa nguvu timu inayoshambulia zaidi kutengeneza nafasi za kufunga kupitia eneo dhaifu la adui.
Kadri mtu anavyokaa kwenye maombi ndivyo anavyozidi kugundua kwa kuoneshwa na Roho Mtakatifu maeneo ambayo adui anakusudia kushambulia kwayo. Ukishakuona hivyo endelea kushambulia.
Maombi hutupa nguvu za kustahimili wakati wa majaribu yetu, maombi ya sasa ni muhimu sana kwaajili ya hali yetu kiroho sasa na wakati ujao. Sasa hii haimaanishi kwamba hatutajaribiwa kwakuwa tupo kwenye maombi, NOPE, tutajaribiwa lakini tutakuwa na nguvu za kushinda majaribu, yaani, tutakuwa na nguvu zaidi ya ile nguvu ya majaribu.
Barikiwa!
Social Plugin