Biblia inasemaje
kuhusu namna tunavyoweza kuishinda hali na asili yetu ya dhambi na matamanio ya
mwili? Jawabu ni kwamba ili kuondokana na kuishinda hali hii kuna jambo ni
lazima tuache kulifanya na lipo tunalopaswa kuanza kulifanya mara moja, lakini
hii itawezekana tukiwezeshwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, ni Roho Mtakatifu pekee
mwenye uwezo wa kutufanya tuache matendo maovu na kutenda matendo mema.
Yesu
alisema, pepo mchafu amtokapo mtu hutafuta mahali pa kukaa, akikosa huamua
kurudi kule likotolewa, akikuta pako wazi huingia tena humo pamoja na marafiki
zake. Mathayo 12:43-45.
Mwanafalsafa
Mgiriki wa kale Aristotle Nicomachus, katika moja ya tafiti zake kuhusu fizikia
ya horror vacui, yaani hofu ya OMBWE (uwazi wa kitu, tupu), alihitimisha kwa
kusema "asili huchukia ombwe-nature abhors a vacuum; natura abhorret a
vacuo. Kwamba kani/nguvu mzunguko za asili katika ulimwengu hutaka kujaza kila
mahali panapokuwa wazi.
Unapoacha
kufanya jambo/tabia fulani kwenye maisha yako, tafadhali haraka sana anza
jambo/tabia nyingine mbadala, lisibaki ombwe vinginevyo zile kani mzunguko
zinazochukia ombwe zitakuwekea tabia/jambo lake jipya ama kukurudishia tabia
ileile uliyoiacha.
Hali ya
kuwa na ombwe humkosesha mtu utulivu, humpa mahangaiko mengi hadi pale ombwe
litakapozibwa (mke wa Potifa, sexual urge, Mwz 39:1-16); hata lile jambo
linaloachwa nalo huhangaika kutafuta mahali palipo wazi likae, sasa linapokosa
mahali pa kukaa, huamua kurudi kulekule lilipotoka na huingia hapo tena ikiwa
patakuwa wazi.
Unapoamua
kuacha tabia fulani isiyofaa, mfn ulevi, wizi, tamaa nk, anza tabia nyingine
mpya inayofaa (Zbr 34:14, Ef 4:28), la sivyo ile tabia uliyoiacha itarudi tena.
Watu wengi
hurudia tabia walizoziacha kwasababu ya kutokuanza tabia nyingine mbadala. Kuacha
tabia zisizofaa pasipo kuanza tabia mpya haitoshi, hadi umeanza tabia mpya.(2Tim
2:22)
Barikiwa!
Acknowledgement: Biblical Christianity in African Perspective pg 203
Social Plugin