Kwanini kujikunyata?!
Jinsi unavyojiona na kujisikia ni matokeo ya mtazamo
ulionao. Unaweza kubadilisha hali mbaya uliyonayo kwa kubadilisha mtazamo wako
tu. Mtazamo huamua hali ya mtu na pia hugeuka sababu ya vile alivyo.
Mtazamo wa mtu kuhusu utajiri/umasikini ndiyo sababu ya
utajiri/umasikini wake; mtazamo wa mtu kuhusu uchawi ndiyo sababu ya uchawi
wake; mtazamo wa mtu kuhusu uchawi ndiyo sababu ya kurogwa/kutorogeka kwake;
mtazamo wa mtu kuhusu mke/mume wake ndiyo sababu ya jinsi anavyomchukulia;
kufaulu/kufeli kwa mtu ni matokeo ya mtazamo wa mtu kuhusu mtihani wenyewe.
Vile ulivyo ni mtazamo wako.
Rafiki yako,
Lazaro JP Kavageme
0769-085178/0787-654724
0769-085178/0787-654724
Social Plugin