Tusome kidogo...
Mwaka 1983 Dr Howard Gardener wa chuo kikuu cha Harvard katika kitabu chake cha "Frames of Minds "( Theory of Multiple Intelligence) alileta ugunduzi wa aina nane (8) za uwezo wa mtu ambapo ni mbili tu kati ya hizo zinazopimwa katika mifumo ya kawaida ya shuleni. Aina hizo ni;
1)Verbal-linguistic intelligence (word smart)
2) Logical-mathematical intelligence (number smart)
Aina hizi mbili ndizo zinazoangaliwa sana darasani na ziko katika upande wa kushoto wa ubongo. Muunganiko wa hizo mbili unaonesha kuwa na mchango mkubwa sana darasani.
3. Spatial-intelligence (picture smart). Wako vizuri sana katika imagination na kumbukumbu za picha. Kazi zao ni kama; mpambaji, wapiga picha, usanifu majengo n.k
4.Bodily-kinesthetic intelligence (body smart). Wengi hawa ni wanamichezo, waigizaji n.k wamejaaliwa sana katika matendo.
5.Musical-Intelligence (music smart) . Ni wazuri katika kutumia ala za muziki na ni watunzi wazuri.
6.Naturalist intelligence (nature smart). Aina hii hujali sana mazingira na kupenda wanyama na mimea. Ni wakulima wazuri, wanapenda kuwa na bustani za maua, daktari wa mifugo n.k
7. Intraperson intelligence (self smart). Aina hii imejikita katika kujitambua mtu binafsi. Hufanya mambo kwa ubora sana wanapofanya wenyewe. Wanaweza kuwa washauri wazuri, wapembuzi na wachambuzi (Analysts) n.k
8. Interpersonal intelligence (people smart). Aina hii wako vizuri sana katika mahusiano na watu, hupenda kuchangia mada na midahalo mbali mbali, kufundisha watu n.k wengi ni viongozi wazuri, washauri, makocha wa michezo na wanadiplomasia.
Aina hizi sita za mwisho (3-8) ziko zaidi katika mfumo wa jamii na ziko katika upande wa kulia wa ubongo wa mwanadamu. Baada ya kutambua aina hizi kazi inayobaki ni ya mtu binafsi kutafakari na kuona yeye yuko upande gani na anawezaje kutumia uwezo huo kuweza kufanikiwa.
Kutoka 31:1-4
Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina, ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba,
Social Plugin