TUFANI INAPOVUMA


TENZI NAMBA 117
TUFANI INAPOVUMA

Tufani inapovuma, busara ni kutulia na kufurahia hali ya ushwari upande wa pili. Wavuvi huwa hawaingii majini kuvua wakati wa tufani bali huwa wanatumia muda wa kusubiri tufani ipite kwa kuandaa vifaa vya kazi yao. 

Kila kitu kina pacha, ndiyo asili; tufani na shwari, usiku na mchana, chanya na hasi, utajiri na umasikini, yin na yang, samurai na ninja, nk. Hali hizi zote hutokea kwakuwa zimepangwa kutokea, kuzikabili ni kujirubuni na kutumia vibaya ukweli kwamba hali hizo zipo na ni muda wake kutawala.

Wengi tumenaswa kwenye mtego huu, na kujikosesha furaha; tunajitahidi kuzizuia hali ambazo ni muda wa utawala wake tukidhani kwamba kwa kufanya hivyo ndiyo tunapambania hatima zetu. Msongo wa mawazo na sonona huanzia hapa. Hakuna wazo lenye nguvu kushinda jambo ambalo utimilimilifu wake umewadia. 

Tunaweza kujizoeza kuzikubali hali za maisha na kukubali kuyaishi maisha jinsi yalivyo kiasi tukaifanya furaha kuwa jambo la kawaida kama oxygen.