Nyota

Waafrika wanaoweza kuzisikia nyota.

Katika ulimwengu wa jangwa la Kalahari, Laurens van der Post, anasimulia uzoefu katika maisha yake miongoni mwa watu wa kiasili wa Jangwa la Kalahari wa jamii ya Bushmen. Anaelezea mshtuko wao walipogundua kwamba hawezi kuzisikia nyota kama wao.

Mwanzoni, walidhani alikuwa anatania au anadanganya.  Lakini walipogundua kwamba kweli hakuwa akizisikia, walihuzunika sana. Kwa Bushmen, kutoweza kuisikia asili inahesabika kuwa ndiyo upweke na dhiki kubwa zaidi ambayo mtu angeweza kuwa nayo, kwao ni ishara ya kutengwa sana na ulimwengu unaowazunguka.

Sisi ni sehemu ya ukweli mkuu wa uumbaji kuliko tunavyofahamu. Hili limefundishwa tangu mwanzo wa wakati. Tamaduni nyingi za kiasili zinaishi ukweli huu, ingawa miundo yetu ya kisasa ya kidini, kitamaduni, na kijamii imetutoa kwenye reli na kututupa mbali na ukweli huo wa kiroho. 

Amos 5:8; Ayubu 9:9; Ayubu 38:31-32; Mathayo 2:2; Lk 12:54-56