GenZ

GenZ wamekuja kurekebisha kile Millenials na GenX tulikikosea, they are not trying to survive kama siye tulivyo na tunavyofanya, they are stepping into assignment.

Ufahamu huu unasambaa kwa kasi ya moto wa mwituni. Taasisi nyingi zinatikiswa, naiona hii hadi kanisani, wanatukaba shingoni kwenye mambo mengi, sometimes wanakaa kimya tu kwa kukuheshimu lakini mioyo na nafsi zao zinapiga kelele wakati wote, uwe na hakika hawatakaa kimya kwa muda mrefu, siku inakuja watapiga kelele hadharani ikiwa hatubadiriki. 

Wanatufundisha kwamba power haipo kwenye institutions bali ipo kwenye ufahamu (consciousnes) na ufahamu huumba uhalisia (reality)

Tunajiuliza, hawa wa kwetu waliwezaje kutenda mambo yaliyofanana kwa wakati mmoja kwenye mikoa zaidi ya mitano Tanzania Bara bila hamasa ya picha na video (internet ilizimwa)wala kupigiana simu. Katika hili wanatufunza kwamba muda ni ombwe mipaka unajiwekea mwenyewe tu (time is not linear it is simultaneous) kwamba kila kitu kinaweza kutokea ndani ya muda mmoja kila mahali. Tumeona walichofanya kwenye nchi nyingi, kuzitaja chache, Madagascar, Nepal, na Mexico.

Roho inapokuwa tayari, timeline hubadilika, hakuna kitu chenye nguvu kushinda wazo ambalo utimilifu wake umewadia. 

Huu ni mwito wa kiroho pia, kwamba katika ulimwengu wa kiroho hakuna kitu kinachotokea kwa bahati nasibu (the spiritual realm is not random) Wagalatia 4:4. Mungu anaweka mizani sawa kupitia wao, anataka viongozi ambao ni watumishi wa watu na siyo viongozi wachumia tumbo. Kwa waliojenga juu ya misingi ya rushwa misingi inavunjwa, Yesu alisema "..hakuna neno lililositirika lisifunuliwe.." Luka 12:2-3. Katika hili internet inasaidia sana

Soon wanaanza kuikacha mifumo ya kidini na kukumbatatia kingdom identity (...Ufalme wa Mungu umo ndani yenu, Luka 17:21). Ni movement ya kutafuta ukweli wa kiroho kibinafsi kuliko kutegemea taasisi za kiroho na viongozi wa dini, watu hawakomai kiroho kama hawahoji yale yanayotokea nje yao; hakuna jibu bila swali wala hakuna swali lisilotafuta jibu. Nyakati hizi zinatoa nuru hii kwamba dini kwa sehemu kubwa zinatumika kama nyenzo ya kutawala watu.

Nyakati za uvuvi wa watu zinaishilizia, zinaingia nyakati za mbeba mtungi wa maji (Luka 22:10). Inaonekana mbeba bendera wa nyakati hizi ni GenZ.

Anayechezea nafasi ya kuramba asali ikiwa kwenye kijiko atakujairamba ikiwa kwenye ncha ya kisu.