Katikati ya usiku, kulikuwa na mchungaji huko Chicago ambaye aliamshwa kutoka usingizini. Alimsikia Roho Mtakatifu akimwambia aende kwenye kituo cha treni cha Chicago na kuhubiri Injili. Alijiwazia, “huo ni ujinga. Kwa nini Mungu aniombe nifanye hivyo?” Basi akajipindua na kurudi kulala. Jambo lile lile lilifanyika tena mara ya pili, na kisha mara ya tatu, hadi mwishowe mtu huyo akakubali na akaendesha gari hadi kituo cha treni.
Alipofika hakukuwa na mtu, lakini alikuwa mtiifu na alihubiri ujumbe wa msingi wa Injili na hata kutoa wito wa madhabahuni ingawa ilionekana hakuna mtu anayesikiliza. Baadaye, alienda nyumbani.
Miaka kadhaa baadaye mchungaji huyo huyo alienda kwenye mkutano wa 𝐁𝐢𝐥𝐥𝐲 𝐒𝐮𝐧𝐝𝐚𝐲 ambapo mwinjilisti huyu alitoa ushuhuda wake wa jinsi alivyopokea wokovu. Alisema, “Usiku mmoja nilikuwa chini kwenye kituo cha treni cha Chicago, na kulikuwa na mtu akihubiri Injili, ingawa sikuweza kumwona wala sikujua sauti hiyo ilikuwa inatoka wapi, aliniongoza kwa Bwana usiku huo!” 𝐁𝐢𝐥𝐥𝐲 𝐒𝐮𝐧𝐝𝐚𝐲 aliwafikia mamilioni ya watu kwa Injili kupitia huduma yake.
𝐌𝐮𝐡𝐢𝐦𝐮:
Usimdharau mtu yeyote unayemhubiria au unayemshuhudia – huwezi kujua Mungu atamtumiaje baadaye.
🎯Watu wengi tunaishi kwenye sympathetic (fight/logic/control). Kila kitu kiwe na maana kabla hatujachukua hatua (mkate wenye chachu)
Lakini mwongozo wa Roho unakuja zaidi kwenye parasympathetic (stillness/listening. Hakuna hofu wala mihemko. Ni virgin consciousness (mkate usiotiwa chachu) mfano, Eliya pangoni 1Wafalme 19:1-18; Samweli na Eli, 1Samweli 3:1-10
👉 Funzo:
Unapoingia katika utulivu wa ndani, unaweza kusikia maagizo ambayo akili haiwezi kuyaeleza. Ni hatua ya juu sana inayelekeza:-
🔹Sio kufanya kwa sababu unaelewa
🔹Sio kufanya kwa sababu unaona matokeo
Bali ni kufanya kwa sababu umeamini na unaiamini imani yako
Hii ni aina ya imani ambayo Abraham aliishi nayo—alienda bila kujua anakokwenda.
1 Wakorintho 1:25:
“Kwa maana upumbavu wa Mungu ni wenye hekima kuliko hekima ya wanadamu…”
Social Plugin