Yusufu na Nduguze

Mwanzo 37:23-28, 39:1-20

Kabla hawajamtupa shimoni, walimvua kanzu yake. Kanzu hiyo haikuwa nguo tu. Ilikuwa ni utambulisho wa neema na mali; Ushahidi kwamba alionekana, kuchaguliwa, na kupendwa. 

Jambo la kwanza ambalo ndugu zake walifanya, kabla ya shimo, kabla ya utumwa, kabla ya lolote kati yake….. lilikuwa ni kumvua utambulisho wake. 

Ikiwa unataka kumwangamiza mtu, haumdhuru tu. Unajaribu kuchukua utambulisho wake kwanza.

Baada ya hayo, kila mahali Yusufu alipokwenda, mazingira na watu walijaribu kumpa utambulisho mpya: 
🔹️Utumwa alisema: Wewe ni bidhaa. 
🔹️Mke wa Potifa alisema: Wewe ni fursa (kijana barubaru, kiben10)
🔹️Gereza lilisema: Wewe ni mhalifu. 
🔹️Miaka ya ukimya ilisema: Umesahaulika. 

Uongo mtupu! Hizo ni nafasi nne tofauti kwa Yusufu kuamini alikuwa chochote kile hali yake ilimtambulisha kuwa. Lakini yeye alisema hapana kwa vyote kwakuwa alijua yeye ni nani.

Kumbuka, wewe ni nani!

Unaweza kusalitiwa na bado ukashikilia utambulisho wako. Unaweza kusahaulika; Unaweza kuhukumiwa vibaya, kupewa jina baya, na kutoeleweka, na bado ukashikilia utambulisho wako.

Yusufu alitoka katika kila utambulisho uliolazimishwa kwake na kuingia katika ULE ambao ulikuwa wake kwa kweli siku zote.

Ikiwa mtu alikuvua kitu, cheo, uhusiano, msimu, toleo lako mwenyewe ulilodhani limepotea kabisa, ninahitaji usikie hili…

Wanaweza kuchukua koti. Hawawezi kuchukua wito.