𝐊𝐢𝐭𝐢 𝐔𝐥𝐢𝐜𝐡𝐨𝐤𝐢𝐤𝐚𝐥𝐢𝐚 𝐊𝐰𝐚 𝐌𝐮𝐝𝐚 𝐌𝐫𝐞𝐟𝐮


Kuna aina ya uchovu ambao hautokani na kazi nyingi, wala matatizo mengi. Unatokana na kukaa sehemu moja ya maisha kwa muda mrefu sana huku ndani yako tayari ikijua umeipaswa kuondoka.

Watu wengi hawaelewi kuwa maisha yana “viti.” Kuna kiti cha mwanafunzi, kiti cha mpambanaji, kiti cha mwenye majeraha, kiti cha mtu anayejificha, hata kiti cha mtu aliyekuwa version ya zamani yake. Tatizo si kukaa kwenye kiti, tatizo ni pale ambapo maisha tayari yanataka usimame, lakini wewe bado umekishikilia kwa sababu kinakufanya ujisikie salama.

Na kadri unavyokaa kwenye kiti kisichokufaa tena, ndivyo unavyoanza kuhisi uzito usioeleweka.

Unakuwa bored na vitu ulivyovipenda zamani. Mazungumzo hayakupi tena ule mzuka. Sehemu ulizokuwa comfortable zinaanza kukunyima amani. Sio kwa sababu umeharibika bali ni kwa sababu nafsi yako imeanza kukua kuliko mazingira uliyokaa ndani yake.

Lakini watu wengi huogopa kusimama. Kwa sababu kusimama kunamaanisha kuacha identity waliyoizoea. Inamaanisha kuingia sehemu ambayo bado hawajajua wao ni nani humo.

Ndiyo maana wengine hubaki kwenye mahusiano yaliyokufa, kazi zisizo na uhai, au version za zamani zao, si kwa sababu wanazipenda sana, bali kwa sababu wanaogopa kile kinachokuja baada yake.

Kuna wakati maisha hayahitaji ujifunze kitu kipya kwanza.

Yanahitaji ukubali kuwa tayari umepitwa na kile ulichozoea. Hii ndiyo hatua ngumu zaidi ya ukuaji. Kwa sababu hakuna mtu anayependa kuachana na kitu kilichowahi kumpa comfort, hata kama sasa kinamzuia.

Na kitu cha ajabu ni hiki: Ukikalia kiti kisichokufaa muda mrefu sana, utaanza kufikiri uchovu wako ni personality yako. Utafikiri wewe ni mtu aliyepotea, aliyebadilika, au aliyekuwa empty. Kumbe si kweli. Ni mazingira yako hayalingani tena na ukubwa wa ndani yako.

Ndiyo maana wakati mwingine mabadiliko makubwa hayaanzi kwa kupata kitu kipya. Yanaanza kwa kusimama kutoka kwenye kiti cha zamani. Kwa sababu huwezi kuona maisha mapya ukiwa bado umekalia nafasi ambayo ilitengenezwa kwa version yako ya zamani.

Na somo kubwa hapa ni hili: Usiogope kusimama kutoka sehemu iliyokufariji zamani. Wakati mwingine discomfort unayoihisi si ishara kwamba unapotea, ni ishara kwamba umekua.