𝐍𝐞𝐮𝐫𝐨𝐭𝐡𝐞𝐨𝐥𝐨𝐠𝐲


𝐀
Utafiti wa kisayansi uliofanywa na Chuo Kikuu cha Harvard, Marekani, uligundua kuwa wagonjwa ambao waliombewa walipata nafuu haraka kuliko wale ambao hawakuombewa, hata kama hawakujua sala hiyo.
𝐁
Neurotheology ni tawi ya utafiti inayochunguza uhusiano kati ya ubongo wa binadamu na uzoefu wa kiroho au kidini. Kwa Kiswahili rahisi, ni sayansi inayochunguza jinsi ubongo unavyohusika au kuathiriwa na imani za kidini, sala/maombi, na tafakari (meditation).

Neno "Neurotheology" linatokana na maneno mawili:

"Neuro" – linalohusiana na ubongo na mfumo wa neva.

"Theology" – linalohusiana na masuala ya Mungu, dini, au imani ya kiroho.

Neurotheology inajumuisha taaluma kama Neuroscience (sayansi ya ubongo), Saikolojia, na Theolojia (teolojia).

Watafiti wa Neurotheology huuliza maswali kama:

1. Ni nini hutokea kwenye ubongo mtu anaposali au anapotafakari (meditate)?

2. Je, kuna tofauti katika ubongo kati ya watu wanaoamini (waumini) na wasioamini (wasiomjua Mungu)?

3. Tafakari na sala huchochea sehemu zipi za ubongo?

𝐌𝐛𝐢𝐧𝐮 𝐳𝐚 𝐔𝐭𝐚𝐟𝐢𝐭𝐢
Wataalamu hutumia vifaa kama:
fMRI (functional Magnetic Resonance Imaging) – kuchunguza sehemu ya ubongo inayofanya kazi wakati wa sala au tafakari.

EEG (Electroencephalogram) – kupima shughuli za umeme kwenye ubongo wakati mtu anasali au kuimba nyimbo za ibada.

Dr. Andrew Newberg kutoka University of Pennsylvania, Marekani aliwaalika watawa wa Kibudha na Watawa Wakristo waliobobea kwenye sala na tafakari.

Wakiwa kwenye kilele cha tafakari na sala (deep spiritual focus), aliwapima kwa kutumia fMRI na SPECT scan – teknolojia ya kuonyesha shughuli ya ubongo. Matokeo ya Utafiti huo yalionesha..

1. Kuongezeka kwa shughuli kwenye sehemu ya mbele ya ubongo (frontal lobe) – inayohusika na umakini, nia, na maamuzi.

2. Kupungua kwa shughuli kwenye sehemu ya nyuma (parietal lobe) – inayohusika na mwelekeo wa mwili na nafasi. Hii ilihusishwa na hisia ya “kufuta mipaka kati ya mtu na ulimwengu” – hii ni hali ya kiroho inayomuunganisha mtu na asili/kiini chake (Mungu)

3. Utafiti ulionesha kuwa sala au tafakari ya kina huleta amani, upendo, na hali ya kuwa huru kiakili – hali inayoweza kuathiri tabia ya mtu kwa njia chanya.
𝐂
Neurotheology na Tiba ya Msongo wa Mawazo (Stress, Anxiety, Depression)

Tafiti zinaonyesha kuwa sala ya kina na tafakari (meditation) hupunguza viwango vya cortisol, homoni ya msongo wa mawazo.

Wagonjwa wa sonona waliowekwa kwenye mpango wa kutafakari kiroho waliripoti kupata amani, matumaini, na mwelekeo wa maisha.

Kliniki nyingi za afya ya akili sasa zinaongeza vipindi vya tafakari au maombi kama sehemu ya tiba (mind-body therapies).

𝐇𝐢𝐭𝐢𝐦𝐢𝐬𝐡𝐨
Tafakari na sala huathiri ubongo kwa njia za kupimika kisayansi.

Hisia za kiroho si tu imani za rohoni, bali zina mlingano wa kibaolojia kwenye ubongo na mfumo mzima wa neva (central nervous system).

Usiache kufanya sala, usiache kutafakari, usiache kuombea wagonjwa.