Funzo kutoka kwa Lidia; Matendo 16:14-15
Mungu huanza na moyo kabla ya majukumu.
Kisa cha Lydia kinafunua siri ambayo watu wengi huikosa:
Mafanikio ya nje hayaondoi uhitaji wa mabadiliko ya ndani.
Alikuwa tayari:-
🌿Ana kipato
🌿Ana heshima
🌿Ana mtandao wa watu
Lakini bado Maandiko yanasema wazi kuwa:
👉 “Bwana alifungua moyo wake…” (Matendo 16:14)
Hapa kuna hatua ya kiroho ambayo ni muhimu sana:
1. Kufunguliwa kwa moyo ni kazi ya Mungu, lakini kunahitaji utayari wa mtu
Lydia alikuwa anasikiliza. Hakuwa amefunga nafsi yake kwa sababu ya mafanikio yake.
Watu wengi wakishafanikiwa, huacha kusikia—lakini yeye alianza kusikia zaidi.
2. Imani ya kweli haiishi moyoni tu, inatafuta mlango wa kutoka
Baada ya kuamini:
Nyumba yake ikawa madhabahu
Biashara yake ikawa chombo
Rasilimali zake zikawa huduma
Hii inaonesha kitu cha kina:
👉 Kila baraka isiyounganishwa na kusudi hugeuka kuwa mzigo wa kimya.
3. Mungu hakubadilisha mazingira yake—alibadilisha mwelekeo wa moyo wake
Hii ni hekima kubwa sana.
Watu wengi wanataka kubadilisha kazi, mji na mazingira.
Lakini Mungu mara nyingi huanza na:
👉 mtazamo (orientation), siyo location
Tafakari kwa kina (kwa roho yako)
Kwako msomaji; Je, moyo wako bado una nafasi ya kushangazwa na Mungu?
Au tayari umejaza majibu kabla hujauliza maswali?
Je, mafanikio yako yamekufanya uwe wazi zaidi… au umejifunga zaidi?
Hitimisho
Lydia anatufundisha kwamba:
Moyo uliofunguliwa na Mungu hauishii kupokea—huanza kuwa mlango wa wengine kuingia kwenye neema.
𝑲𝒂𝒗𝒂𝒈𝒆𝒎𝒆 𝑳𝑱𝑷
𝑰𝒏𝒖𝒌𝒂 𝑻𝒖𝒐𝒏𝒅𝒐𝒌𝒆
Social Plugin