Watu wengi wanafikiri wanapiga picha ili kunasa kile wanachopenda. Lakini angalia kwa karibu, na utagundua kitu zaidi: tunapiga picha kile tunachoogopa kupoteza.
Fikiria hivi, tukiwa out, tunapiga picha kwa shauku sana machweo ya jua, ufukwe, barabara za jiji na chakula cha mchana au jioni cha familia au marafiki. Kwa nini? Kwa sababu tunajua ni vya muda mfupi, na punde tu hatutakuwa hapo tena.
Tayari tunahuzunika kwa ndani, hata tunapotabasamu mbele ya kamera. Ndani yetu tunaelewa kuwa kicheko kwenye meza hiyo au mandhari nzuri za kuvutia, hata ile hisia ya kuwa huru na kujiliwaza kutokana na mazonge ya maisha ya kila siku ... yote hupotea kama ilivyokuja.
Jambo hilo hilo hufanyika katika siku za kuzaliwa, harusi, na kuhitimu masomo. Tunashikilia simu ili kurekodi mtoto wetu akitembea kwenye jukwaa au rafiki wa karibu akisema "Ndiyo, ninakubali," pale anapovishwa pete ya uchumba ama ya ndoa, si kwa sababu tunalipenda sana tukio hilo, bali ni kwa sababu tunaogopa si la kudumu.
Kila picha tunayopiga ni ukiri kwamba:-
๐ฟ"๐๐๐ฃ๐ ๐๐ค๐๐ช ๐ฃ๐๐ฉ๐๐จ๐๐๐๐ช ๐๐๐ก๐"
๐ฟ"๐๐๐ฃ๐ ๐๐ค๐๐ช ๐๐๐ก๐ ๐๐๐ ๐๐ฉ๐๐๐๐๐๐ก๐๐ ๐ ๐ข๐ช๐๐ ๐จ๐ ๐ข๐ง๐๐๐ช"
๐ฟ"๐๐๐ฃ๐ ๐๐ค๐๐ช ๐ ๐ช๐ฌ๐ ๐จ๐๐ฉ๐๐ฌ๐๐๐ ๐ ๐ช๐ฌ๐ ๐ฃ๐ ๐๐ช๐ง๐๐๐ ๐ ๐๐ข๐ ๐๐๐ ๐ฉ๐๐ฃ๐"
๐ฟ"๐๐๐ฃ๐ ๐๐๐๐ช ๐จ๐๐ฃ๐ฉ๐๐ฅ๐๐ฉ๐ ๐๐๐๐ ๐ช๐ก๐ ๐ ๐๐ข๐ ๐๐๐ ๐ ๐๐๐ซ๐ ๐ ๐๐ง๐๐๐ช๐ฃ๐".
Hatupigi picha tu kukumbuka mambo muhimu. Tunapiga picha kwa sababu tunajua hatuwezi kuwa hapo milele.
Ukitaka kujua kile mtu ana hofia kukipoteza, au kile ambacho hana uhakika kukipata hivi karibuni, basi fuatilia picha anazopiga.
Social Plugin