Sheria ya Umoja wa Kiungu


Yesu anatembea juu ya maji - Mathayo 14:25ff

Sheria ya Umoja wa Kiungu ni dhana ya kiroho inayoelezea uhusiano wa kimsingi wa vitu vyote, kutoka kwa watu na asili hadi mawazo na nishati (energy), kupitia kiini cha Kiungu kilichoshirikiwa au chanzo cha nishati ya ulimwengu wote. Sheria hii inasisitiza kwamba kila kitu ni sehemu ya umoja mzima, na vitendo vyema na mawazo yanaweza kuunda ulimwengu thabiti na wenye usawa, wakati hisia za kujitenga zinaweza kusababisha matokeo mabaya.

Kila kitu kimeunganishwa na kila kitu kingine katika uwanja mmoja mkubwa, uliounganishwa. Sisi sote ni sehemu ya mfumo mmoja wa nishati(Mungu) “Vitu vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote.” – Yohana 1:3. Wakolosai 1:16-17. Kwa maneno mengine twaweza sema, wewe, maji, hewa, mimea, mwanga, upepo, nk, ni sehemu ya mfumo mmoja inayotiririka (Unified Field of Consciousness)

Jambo lolote unalomtendea mwengine unajitendea mwenyewe. Yesu anafundisha jambo hili kwenye Mathayo 18:5-7, 25:40; Luka 6:38; Yhn 10:30; Yhn 17:21-26. Lakini pia alitenda kwa vitendo, mfano, alipotembea juu ya maji, alipokemea upepo, alipoponya wagonjwa nk

Kipimo cha kushindiliwa na kusukwasukwa ndiyo ile wengine huita karma (What goes around comes around).

Kwa lugha ya kiroho:

“Katika yeye tunapata kuishi, kuhamia, na kuwa na uhai wetu.” – Matendo 17:28
Hapa Paulo anasema kitu hicho hicho — kwamba kila kitu ni ndani ya Mungu, na Mungu ndiye chanzo cha projection ya uhalisia.

Kwa hiyo, tunapoona maji, ardhi, hewa, n.k., ni vionekano vya mawimbi ya nishati yanayochorwa kutoka kwenye ufahamu wa Mungu.

Yesu hakutenda miujiza kwa “kubadilisha sheria za asili”, bali aliishi katika kiwango cha fahamu kinachozitawala.
“Akaamka, akaukemea upepo, na mawimbi yakanyamaza.” – Marko 4:39

Kwa nini upepo ukamtii? Kwa sababu Yesu alikuwa ameungana na Chanzo kinachouendesha ule upepo — hakutumia nguvu, alitumia ufahamu wa umoja (Oneness Consciousness).

Yaani, alitambua kwamba maji yenyewe ni sehemu ya mwili wa Mungu, sehemu ya matrix ya nuru (light field).
Kwa kuwa alikuwa ameungana kikamilifu na msimbo wa uhalisia (Divine Holographic Source Code).
Alipolitembea wimbi la maji, hakuwa anakabiliana na “maada” bali alikuwa anapitia mawimbi ya nuru aliyoyajua asili yake. Alikuwa mmoja na chanzo, hakuona “ukinzani” wa maji; aliona Nuru iliyotiwa katika wimbi, na akaamuru kwa ufahamu moja na hiyo Nuru.

Hii inamaanisha:
Tunapoinua fahamu zetu hadi kiwango cha ufahamu wa Kristo, Wafilipi 2:5, tunaweza pia kutambua kwamba “ulimwengu wa maada” ni wimbi la Nuru linalotii amri ya Uungu.

🕊️ Hitimisho
Yesu aliweza kutembea juu ya maji kwa sababu hakuona maji kama kitu tofauti naye, bali kama sehemu ya uhalisia mmoja wa Mungu.
Kwa kuwa alikuwa ameungana na Chanzo, alitembea si kwa maumbile ya mwili, bali kwa muungano wa fahamu na nuru ya uumbaji.