Taarifa Mbili

Kila siku tunapewa taarifa mbili za kuchagua ili kuzifanyia kazi, tunapewa taarifa mbaya na taarifa nzuri kwa wakati mmoja. Kwenye kitabu cha Wafalme 1 sura ya 19:1-2, Yezebeli alipewa taarifa mbili na Ahabu mumewe, mfalme wa Israeli. Taarifa ya maombi ya Eliya hadi mvua ikanyesha na taarifa ya kuchinjwa kwa manabii wa Baali; Yezebeli alichagua kufanyia kazi taarifa mbaya ya manabii kuuawa, na kwahivyo akajiapiza kumuua Eliya nabii.

Taarifa nzuri zinatuvuta kumshukuru Mungu na hivyo kufungua milango ya kumuona Mungu katika mwanga bora zaidi. Taarifa mbaya zinatuvuta kufanya ubaya na hivyo hufunga uwezekano wa kuona mema ndani ya ubaya huo. 

Ayubu akamuuliza mkewe, ..Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Ayubu 2:10b

Mungu anawasiliana nasi kupitia taarifa zote mbili. Hata kwenye taarifa mbaya lipo funzo ka la maisha yetu.