IMANI YA NIKEA

Imani ya Nikea ni mojawapo ya imani maarufu na yenye ushawishi mkubwa katika historia ya kanisa, hii ni kwa sababu ilitatua swali la jinsi Wakristo wanaweza kumwabudu Mungu mmoja na pia kudai kwamba Mungu huyu ni nafsi tatu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.

Pia ilikuwa imani ya kwanza kupata mamlaka ya ulimwengu mzima katika kanisa, na iliboresha lugha ya Imani ya Mitume kwa kujumuisha taarifa maalum zaidi kuhusu uungu wa Kristo na Roho Mtakatifu.

MUKTADHA WA KIHISTORIA WA IMANI YA NIKEA:

Kile tunachokiita Imani ya Nikea kwa kweli ni zao la mabaraza mawili ya kiekumene—moja huko Nicea (Iznik ya sasa, Uturuki) mnamo AD 325, na moja huko Constantinople (sasa Istanbul) mnamo 381 BK.

Baraza hilo liliitishwa kutatua tatizo lililozuka miaka saba kabla na kuliacha kanisa la Kikristo likiwa limegawanyika vikali.  Huko Aleksandria mnamo mwaka 318 BK, kasisi mmoja aitwaye Arius alianza kutangaza hadharani nadharia yake kwamba Yesu hakuwa Mungu hata kidogo, ila ni mtumishi wa mbinguni wa Mungu Mkuu wa kweli, ambaye peke yake ndiye mwenyezi, muweza wa yote, muumbaji na sababu ya kwanza ya vitu vyote.

Hoja ya Arius ilifafanuliwa hivi, Yesu alielekea kuwa na hisia-moyo (kinyume na Baba, ambaye sikuzote alikuwa akitawala hisia zake), akakua na kujifunza (kinyume na Baba, ambaye hakubadilika kamwe), na akafa (kinyume na Baba, ambaye  hawezi kufa).

Kwa hiyo, ni Baba pekee anayeweza kuonwa kuwa hajaumbwa na “mwenye kujikimu bila mipaka ya wakati.”

Arius alifikiri kwamba tafsiri yake ilikuwa na msingi mzuri katika theolojia ya mwalimu mkuu Origen. Origen alikuwa amesema kwamba Baba alistahili utukufu na heshima kama Mungu mwenyewe (autotheos) ambayo haikutokana na Mwana.

Askofu wa Arius, Alexander, alikataa, akionyesha kwamba Origen pia alisema "Baba" ni sifa ya milele ya Mungu. Hili linamaanisha kwamba, kwa kuwa haiwezekani kuwa baba bila pia kuwa na watoto, uhakika wa kwamba Mungu ni baba milele unamaanisha kwamba ana mwana milele.

Katika kujaribu kuhifadhi hadhi ya Baba, Arius alikuwa akichezea baadhi ya tofauti muhimu zinazomtenganisha Mungu na wanadamu, akirejea baadhi ya Maandiko 
yanayoonesha Yesu mwenyewe kupendekeza kwamba yuko chini ya Baba (kwa mfano, Yohana 14:28).  Wakati huo huo, Maandiko yako wazi kwa usawa kwamba Yesu anadaiwa kuwa wa kimungu na sawa na Baba kama Mungu (Yohana 1:1; 5:16–18; 10:30; 14:6–14).

Baada ya miaka mingi ya mgawanyiko mkali ambao ulianzia kwa makasisi (Wachungaji)hadi watu wa kawaida, baraza la kiekumene liliitwa kusuluhisha suala hilo mara moja.

IMANI YA NIKEA INASEMA NINI KUHUSU UHUSIANO KATI YA YESU NA BABA:

Tofauti kuu kati ya imani hii na Imani ya Mitume, hata hivyo, ni sehemu mpya, iliyopanuliwa juu ya uhusiano kati ya Yesu na Baba, kwa kuwa hangaiko kuu la baraza lilikuwa kutetea uungu wa kweli wa Mwana dhidi ya mafundisho ya Arius.  Imani inathibitisha hilo kwa kudai “Bwana Yesu Kristo” kuwa “Mwana wa Mungu,” “mzaliwa wa pekee wa Baba,” “mzaliwa-pekee.”  Haya ni madai ya kibiblia (Marko 1:1 na 1 Yoh 4:15 humwita Yesu Mwana wa Mungu; Mdo. 13:33 na Ebr. 5:5 humtaja kama mzaliwa wa Baba; Yoh. 1:14 na 3:18. tumia neno la Kigiriki monogenous, linalomaanisha "mzaliwa-pekee".  Yesu, ni Mungu: “Mungu kutoka kwa Mungu.” hajaumbwa wala si bidhaa ya Mungu wa kweli".

Ilikubaliwa ifahamike wazi kwamba uungu wa Yesu ni uungu wa Baba. Yesu huyo yupo milele na milele “mwili mmoja na Baba.”  Kwa kusisitiza kwamba Mwana ni “mwili mmoja” na Baba, maoni ya Waarian yalikataliwa na baraza hilo likathibitisha kwamba Baba si “Mungu zaidi” kuliko Mwana.  Mungu ni Mungu, katika utatu.

L Kavageme
Inuka Tuondoke Ministries 
Mwanza - TZ