BUNDI

Bila shaka umewahi kusikia na pengine tayari kwa kusikia kule unaamini (Basi imani, chanzo chake ni kusikia; Warumi 10:17)kwamba bundi ni ndege anayeleta balaa kwenye miji ya watu, na amekuwa akitumika kama alama ya mkosi na balaa. Lakini imani hiyo ni kubwa kutokana na kutumika zaidi na walozi kwenye majukumu yao ya kishirikina kama ilivyo kwa paka mweusi au paka mweupe. Kwa hivyo bundi anapolia hasa nyakati za usiku watu hukosa amani na kuamini kuna jambo baya litatokea hasa msiba.

Ukweli ni kwamba kiasili bundi si ndege mwenye kubeba mikosi, wala hana uwezo wa kusababisha msiba. Kilichopo ni kwamba ndege huyu ameumbwa na uwezo mkubwa wa kunusa harufu ya mzoga kwa umbali sana na husogea hadi eneo ulipo mzoga ili ajipatie chakula, ni sehemu ya harakati za mawindo yake. 

Kisayansi, wataalamu wanasema mwanadamu anayekaribia kufa, kinachoanza kufa kwanza huwa ni seli katika viungo vya muhimu zaidi mwilini. Viungo hivi vinapokufa huanza kutoa harufu, harufu ambayo si rahisi binadamu kuilewa, anaweza kusikia na asiielewe ama asiisikie kabisa; lakini bundi yeye husikia harufu hii na ndiyo hiyo humvuta kuja eneo inapotokea na hatimaye hutua juu ya paa la nyumba mgonjwa alipo, na akiwa hapo huanza kulia, kule kulia kwa bundi hakuchochei wala kuharakisha kifo cha mtu bali huashiria furaha na shauku kwakua amekaribia kupata chakula chake. 

Kwanini mara nyingi iwe usiku tu na si mchana? Ni kwasababu usiku ndiyo muda wake wa kufanya mawindo na ndiyo muda anapokua active zaidi ya muda mwingine kwa siku, kama ilivyo kwa popo, mende na viumbe wengine kwenye kundi la Nocturnal. Lakini pia wapo viumbe ambao huwa active nyakati za alfajiri na jioni, mfano Dubu na Sungura, hawa wapo kundi linaitwa Crepuscular.

Mwanga wa jua au giza la usiku huchochea kitu kinaitwa circadian rhythm/circle, huu ni mzunguko unaotawala tabia na saikolojia ya viumbe ndani ya saa 24, imetajwa pia kua ni saa ya ndani ya kiumbe, sasa hii ndiyo huamua saa za uactive wa kiumbe.

Binadamu kwa ujumla muda wake kuwa active ni alfajiri hadi usiku, binadamu anakaa na viumbe wengine kwenye kundi la viumbe wanaoitwa Diurnal kama wengi wanavyompanga, japo kwa upekee wake binadamu anafiti kwenye makundi yote matatu, yaani Diurnal, Crepuscular,  na Nocturnal. Na ndani ya muda huo wa alfajiri hadi usiku tunatofautiana u-active wetu, kwanini, kwasababu binadamu tofauti  na viumbe wengine yeye ni mwili, roho, na nafsi(akili/mtu wa ndani) vyote hivi hutegemeana katika kukamilisha jambo. Kwahiyo tunatofautiana, wapo ambao muda wao wa kuwa active ni saa za alfajiri, wengine saa za asubuhi, wengine saa za mchana, wengine saa za jioni na wengine ni usiku kama bundi. 

Angalia, kuanzia wanafunzi, watunzi wa nyimbo na muziki, waandishi, washairi, wagunduzi, wahunzi; hadi maombi na tahajudi (meditation), hawa wote huwa na muda wao maalumu wa kuwa active kiroho au kimwili au kiakili.

Utajuaje! Angalia muda ambao huwa unakuwa na nguvu zisizo za kawaida katika kufanya kazi hasa zile zinazokutaka kutumia akili nyingi kuliko nguvu au nguvu na  akili kwa pamoja. Kuhusu maombi na tahajudi pia ni vile vile, si kila muda unaweza kuomba katika mtiririko mzuri, Yesu aliamka alfajiri kuomba, Marko 1:35, wengine huomba jioni, wengine usiku wa manani.

Bundi sio kielelezo cha mkosi, ni ndege tu, sema walozi humtumia kwenye shughuli zao za kishirikina kama ilivyo kwa paka mweusi au paka mweupe.