𝗞𝗲𝗻𝗴𝗲𝗹𝗲 𝗬𝗮 𝗦𝗵𝘂𝗹𝗲

𝐊𝐞𝐧𝐠𝐞𝐥𝐞 𝐲𝐚 𝐒𝐡𝐮𝐥𝐞.
𝐀𝐭𝐡𝐚𝐫𝐢 𝐲𝐚 𝐌𝐮𝐤𝐭𝐚𝐝𝐡𝐚 (𝐂𝐨𝐧𝐭𝐞𝐱𝐭 𝐞𝐟𝐟𝐞𝐜𝐭)

Hii ni moja ya dhana muhimu katika saikolojia ya utambuzi (cognitive psychology). Inaeleza jinsi mazingira, hali, wakati, au vitu vinavyotuzunguka vinavyoathiri jinsi tunavyoona, kuelewa, kukumbuka, au kuhukumu kitu fulani.

Kengele ya shule inaweza kukasirisha sana inapolia saa mbili asubuhi (kuanza vipindi), lakini kengele hiyo hiyo inaweza kusikika kama muziki mzuri inapolia saa tisa alasiri(kumaliza vipindi). Ni kengele ile ile, sauti ile ile, hakuna kilichobadilika. Kengele haijabadilika, wewe ndiye uliyebadilika kulingana na wakati na matarajio yako.

Hii inatufundisha kitu muhimu sana:
Tunaweza kubadilisha "maana" tunayolipa tukio lolote kwa kubadilisha mtazamo wetu.

Furaha na hasira nyingi zinazotokea si kutokana na kilichotokea, bali ni maelezo tunayojipa ndani ya akili yetu kuhusu kilichotokea.

Wakati mwingine, kitu kinachotuudhi sana ni kwa sababu tunakiona kama "mwisho wa starehe" (kama kengele ya asubuhi), na kitu kinachotufurahisha ni kwa sababu tunakiona kama "mwisho wa shida" (kama kengele ya alasiri).